• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Afrika na Umoja wa mataifa waunga mkono utekelezaji wa makubaliano ya amani ya Sudan Kusini

  (GMT+08:00) 2018-10-11 08:57:02

  Umoja wa Afrika na Umoja wa mataifa wamesisitiza msimamo wa kuunga mkono utekelezaji wa makubaliano ya amani yaliyosainiwa mwezi uliopita.

  Pande hizo mbili zilifanya ziara ya pamoja nchini Sudan Kusini kati ya tarehe 7 na 9 Oktoba, na kukutana na maofisa wa serikali, wawakilishi wa wanawake, mashirika ya kiraia pamoja na wanahabari kujadili makubaliano ya amani ya nchi hiyo.

  Kamishna wa amani na usalama wa Umoja wa mataifa Bw Smail Chergui, na naibu katibu mkuu wa Umoja wa mataifa anayeshughulikia operesheni za ulinzi wa amani Bw. Jean-Pierre Lacroix, waliambatana na maofisa wa wa Umoja wa mataifa wanaoshughulikia maswala ya wanawake.

  Bw. Chergui amesema wamefurahishwa na dhamira ya watu wa Sudan Kusini, hasa wanawake, katika kurejesha amani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako