• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • TENISI: Djokovic aanza kwa kicheko Shanghai Masters

  (GMT+08:00) 2018-10-11 09:00:30
  Nyota wa tennis, Novak Djokovic ameanza vizuri mashindano ya Shanghai Masters baada ya kumfunga Jeremy Chardy raia wa Ufaransa kwa seti 2-0.

  Djokovic raia wa Serbia, amepata ushindi wa 6-3 na 7-5 katika mchezo huo uliochezwa kwenye viwanja vya Centre Court.

  Katika mchezo ujao, Djokovic anaweza kupambana ama na Marco Cecchinato anayeshika nafasi ya 16 ya ubora au Hyeon Chung.

  Mashindano ya Shanghai Masters yameanza Oktoba 6, mwaka huu na yatamalizika Oktoba 14, mwaka huu yakichezwa Shanghai.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako