Tayari mastaa wa timu hiyo wanaocheza soka la kulipwa Mbwana Samatta anayekipiga Genk ya Ubelgiji na Simon Msuva anayecheza klabu ya Jadida ya Morocco wameshaungana na taifa stars.
Nae rais wa Uganda Yoweri Museveni jana usiku amekutakana na kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo (Uganda the Cranes) ikiwa inajiandaa kwa safari ya kuifuata Lesotho kwa mchezo wa marudiano wa kufuzu michuano hiyo.
Museveni ametoa shilingi milioni 5 za Uganda kwa kila mchezaji, na shilingi milioni 200 kwa timu nzima kama motisha ili timu hiyo ipate ushindi.
Timu nyingine ya Afrika Mashariki, Harambee Stars ya Kenya imelazimishwa sare ya bila kufungana na timu ya taifa ya Ethiopia katika mchezo uliochezwa jana.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |