• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China iliyotoa ni "mtego wa madeni" au " chapati ya maendeleo"?

    (GMT+08:00) 2018-10-11 18:15:49

    Hotuba aliyoitoa makamu wa rais wa Marekani Bw. Mike Pence ambayo inailaani China kwa kutoa mikopo ya mabilioni ya dola kwenye miundo mbinu ya maeneo ya Asia, Afrika, Ulaya na Latin Amerika ambayo imeziletea baadhi ya nchi zinazoendelea "mtego wa madeni", akitangaza kuwa Marekani itatoa "chaguo" mbadala wa China kwa baadhi ya nchi.

    Kutokana na kupamba moto kwa mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani, madhumuni ya hotuba hiyo ya Bw. Pence ya kuipaka China matope na kuchochea mikwaruzano ni bayana sana.

    Sri Lanka ni mfano unaokaririwa mara kwa mara na vyombo vya habari vya nchi za magharibi wakati vinapotoa propaganda juu ya suala la "mtego wa madeni". Kama Bw. Pence alivyosema, Sri Lanka imebeba madeni makubwa baada ya "Kampuni ya China kujenga bandari ya Hambantota ambayo thamani yake ya kibiashara inatiliwa shaka na watu", "serikali ya China iliiwekea shinikizo serikali ya Sri Lanka ikidai kukabidhiwa udhibiti wa bandari hiyo mpya", ili iweze kutumiwa na jeshi la majini la China kama "Kituo cha kijeshi".

    Lakini ukweli wa mambo ni kwamba, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Benki kuu ya Sri Lanka, mikopo inayotolewa na serikali ya China ilichukua asilimia 10 hivi katika madeni ya kigeni ya serikali ya Sri Lanka, na asilimia 61.5 ni mikopo yenye masharti nafuu iliyo chini ya kiwango cha riba cha soko la kimataifa. Hivyo waziri mkuu wa Sri Lanka Bw. Ranil Wickremesinghe ametangaza hadharani kuwa, Sri Lanka haijaingia kwenye "mtego wa madeni" ya China. Amesema mradi wa Bandari ya Hambantota ni mradi wa ushirikiano unaofanyika juu ya msingi wa usawa na kunufaishana, tena unafuata kanuni za kibiashara, ambao unalenga kuijenga bandari hiyo iwe kituo cha usambazaji wa vitu kwenye Bahari ya Hindi, kuhimiza maendeleo ya uchumi wa nchi hiyo, na mawasiliano ya miundo mbinu katika kanda hiyo. Inadakiriwa kuwa hadi ifikapo mwaka 2020, pato la bandari hiyo litachukua asilimia 40 ya pato la serikali ya Sri Lanka, na kutoa nafasi elfu 10 za ajira za moja kwa moja, na nyingine elfu 60 ambazo si za moja kwa moja. Watumiaji wa mtandao wa Internet wa nchi hiyo wanaona kuwa hili ni jambo chanya lililotokea nchini humo.

    Kwa kweli, miradi yote ya ushirikiano inayofanyika kati ya China na nchi zinazoendelea kwa kufuata kanuni ya "kujadiliana, kujenga na kunufaika kwa pamoja", ni "chapati inayoleta maendeleo". Hadi kufikia mwezi Septemba mwaka huu, China imesaini nyaraka 149 za ushirikiano kati ya serikali za nchi 105 na mashirika 29 ya kimataifa yanayojiunga na "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Kati ya mwaka 2013 hadi 2017, thamani ya uagizaji na uuzaji nje wa China na nchi zinazojiunga na pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" imefikia dola trilioni 4.8 za kimarekani, hili ni ongezeko la asilimia 4 kwa mwaka.

    China inafuata kanuni hizo ikifanya ushirikiano na Afrika, vilevile kwa nchi nyingine duniani.  

    Waziri wa uchumi na fedha wa Djibouti Bw. IIyas Moussa Dawaleh ameeleza kuwa, "Hakuna mtu anayehitaji kuwa na wasiwasi juu ya uwekezaji wa China au mtu yeyote, maendeleo ya Djibouti yanapaswa kuamuliwa na serikali ya Djibouti, hayahusiani na ajenda yoyote ya kisiasa ya nchi yoyote."

    Bw. Pence alisema kwenye hotuba yake kwamba, Marekani "itatoa chaguo lililo la haki na wazi kwa baadhi ya nchi", lakini watu wanavyoona ni kwamba, nyuma ya "uwongo "ulioahidiwa na serikali ya Marekani, kuna kanuni yake ya umwamba inayoishikilia ya "Marekani Kwanza". Kama mkuu wa Benki ya kimataifa ya Njia ya Hariri ya Djibouti alivyodhihirisha" Marekani iliingia nchini Djibouti mapema zaidi kuliko China, lakini hadi sasa imeiletea nini nchi hiyo? Hapana."

    Katika mchakato wa ushirikiano na nje kati ya China na Marekani, watu wanaweza kufahamu vizuri kanuni zilizopewa kipaumbele na rais Xi Jinping wa China katika Mkutano wa viongozi wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika", nazo ni pamoja na "China haitaingilia kati nchi za Afrika katika kutafuta njia ya kujiendeleza inayolingana na hali ya nchi yake, kutoingilia kati mambo ya ndani ya Afrika, kutolazimisha nchi za Afrika kwa maslahi yake, kutoweka masharti yoyote ya kisiasa katika utoaji wa misaada kwa Afrika, na kutojitafutia faida za kisiasa katika mafungamano na uwekezaji barani Afrika".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako