• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga hatua yoyote za kujilinda kibiashara na vigezo viwili

    (GMT+08:00) 2018-10-11 18:46:37

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang amesisitiza tena kuwa China inapinga hatua yoyote ya kujilinda kibiashara na matumizi ya vigezo viwili.

    Lu Kang amesema, China inaipongeza Canada kwa msimamo wake kuhusu "Makubaliano kati ya Marekani, Mexico na Canada" kwamba hayawezi kuharibu maslahi halali ya nchi nyingine, na nchi hiyo itahimiza mazungumzo ya makubaliano ya biashara huria na nchi nyingi kutokana na uamuzi wake.

    Mjumbe wa taifa wa China ambaye pia waziri wa mambo ya nje Bw. Wang Yi hivi karibuni amefanya mazungumzo na mwenzake wa Canada Bibi Chrystia Freeland kwa njia ya simu. Bibi Freeland amefafanua kuhusu "Makubaliano kati ya Marekani, Mexico na Canada", huku akisisitiza kuwa nchi hiyo itahimiza mazungumzo ya makubaliano ya biashara huria na nchi nyingi kutokana na uamuzi wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako