• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya:Benki ya dunia yaonya Kenya dhidi ya kupunguza bajeti ya maendeleo

  (GMT+08:00) 2018-10-11 19:45:26

  Benki ya dunia imeionya Kenya kwa kupunguza bajeti ya miradi ya maendeleo na kuendelea kukopa kwa ajili ya kufadhili serikali za kaunti.

  Benki hiyo kupitia kwa mmoja wa wanauchumi wake Peter Chacha ,imesema uamuzi huo utasuluhisha matatizo ya ukosefu wa fedha kwa mda tu, lakini utaacha athari mbaya kwa siku ya baadae.

  Kufuatia ukosefu wa fedha za kutosha nchini Kenya,serikali imeamua kupunguza fedha za miradi ya miundo msingi kama barabara na viwanda, jambo litakalochangia watu kupoteza ajira.

  Duku duku la benki ya dunia linajiri mwezi mmoja tu baada ya serikali ya Kenya kuzuia shilingi bilioni 34.33 za maendeleo.

  Ripoti ya hivi karibuni ya benki hiyo,inaonyesha kwamba matumizi ya fedha za miradi muhimu yamepungua kwa asilimia 8 mwaka huu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako