• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ethiopia:Wageni kutoka nchi za Afrika kupewa visa wanapowasili tu

  (GMT+08:00) 2018-10-11 19:50:05

  Ethipia imejitolea kuongoza harakati za uhuru wa kutembea na biashara barani Afrika.

  Nchi hiyo sasa itawaruhusu wananchi kutoka nchi za Afrika kuingia nchi hiyo bila ya kuwasilisha maombi ya utaratibu mrefu wa visa na badala yake kupewa visa wanapowasili tu nchini humo.

  Hatua hiyo ya waziri mkuu wa nchi hiyo Abiy Ahmed aidha itaidhinisha visa kupitia kwa mtandao kutoka kwa raia kutoka nchi tofauti duniani.

  Addis Ababa ikiwa moja ya jiji maarufu kwa kuwa na afisi kuu ya Umoja wa Mataifa inatarajia kujiongezea idadi ya watalii kwa jambo hili.

  Tangazo hili vile vile limempa sifa na heshima waziri huyo mkuu mpya na kufungua fursa kede kede za uwekezaji na biashara.

  Huenda pia jambo hili likashinikiza nchi nyingine za Afrika kufuatia mkondo huo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako