• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania:Wakulima wa mbaazi wapata soko jipya

  (GMT+08:00) 2018-10-11 19:50:24

  Wakulima wa Mbaazi na Choroko wamepata habari njema baada wawekezaji kujitokeza kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya kuchakata mazao hayo nchini.

  Viwanda hivyo vinatarajiwa kujengwa katika mikoa ya Arusha, Dodoma, Dar es Salaam na Morogoro. vitatumia mbaazi na choroko kutoka kwa wakulima kwaajili ya kutengeneza bidha mbalimbali zitakazouzwa ndani na nje ya nchi.

  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Dk Ashatu Kijaji amesema Wilaya ya Kondoa ina wakulima wengi ambao wanahitaji kuboreshewa mazingira yao ya kilimo ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuchangia katika pato la Taifa.

  Bei ya Mbaazi iliimarika katika msimu wa mwaka 2015 ambapo kilo moja ilikuwa ikiuzwa kwa Sh2,800 hadi 3,000 (sawa na 280,000-300,000 kwa gunia la kilo 100) ambapo ilikuwa neema kwa wakulima na msimu uliofuata wa 2016 uzalishaji uliongezeka zaidi lakini matatizo ya soko yakaanza kujitokeza.

  Tanzania ni moja ya nchi za Afrika zinazozalisha kwa wingi mbaazi, ambapo asilimia 95 ya zao hilo ilikuwa inauzwa nchini India na sehemu ndogo iliyobaki inatumika kwa chakula.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako