• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Watanzania waungana na Simba SC wamlilia Mo

  (GMT+08:00) 2018-10-12 08:33:09
  Watanzania wameungana na viongozi, wachezaji na mashabiki wa klabu ya Simba ya Dar es salaam kuguswa na tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara kijana barani Afrika na mfadhili wa klabu hiyo Mohamed Dewji "Mo".

  Mo alitekwa jana asubuhi wakati akielekea kufanya mazoezi ya viungo (gym) katika hoteli ya Colosseum iliyopo jijini Dar es salaam.

  Kwa mujibu wa kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa amesema Mo ametekwa na raia wawili wa kigeni.

  Kwa upande wa klabu ya Simba kupitia kwa msemaji wake Haji Manara, imewataka wanachama na mashabiki wake kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho vyombo vya dola vinafanya jitihada kuhakikisha Mo anapatikana akiwa salama.

  Nayo klabu ya Yanga imesema ukiachana na masuala ya utani wa jadi, imeguswa na kusikitishwa na taarifa za kutekwa kwa Mo ambaye ni mtu muhimu kwa watani wao Simba pamoja na mpira wa Tanzania, hivyo inamuombea kheri huko aliko na apatikane akiwa salama.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako