• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya, Ethiopia zaingia vitani kusaka nafasi ya kufuzu AFCON 2019

  (GMT+08:00) 2018-10-12 08:34:09
  Timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars jumapili hii inahitaji kujiweka nafasi nzuri ya kufuzu fainali ya michuano ya AFCON 2019 itakayofanyika nchini Cameroon.

  Mechi hiyo ya marudiano baada ya mechi ya kwanza kuchezwa jijini Addis Ababa juzi jumatano na timu hizo kutoka sare ya bila kufungana. Matokeo hayo yanaiweka Kenya katika nafasi nzuri zaidi ambayo inaongoza Kundi F, ikifuatiwa na Ethiopia. Ghana ni ya tatu huku nafasi ya nne ikishikwa na Sierra Leone ambayo imefungiwa na shirikisho la soka duniani FIFA kutojihusisha na masuala ya soka kwa muda usiojulikana.

  Ethiopia pia ina nafasi nzuri ya kufuzu endapo tu itafanikiwa kuifunga Kenya katika mchezo huo wa marudiano utakaopigwa jijini Nairobi Kenya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako