• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa UM asisitiza haja ya kuondoa "nguvu hasi" kwenye eneo la maziwa makuu

    (GMT+08:00) 2018-10-12 08:57:13

    Mjumbe maalumu wa Umoja wa mataifa katika eneo la maziwa makuu Bw. Said Djinnit, amesisitiza haja ya kuondoa "nguvu hasi" kwenye kanda hiyo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kutuliza hali nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC.

    Akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la usalama la Umoja wa mataifa kuhusu suala la DRC, Bw. Djinnit amesema kukosekana kwa usalama mashariki mwa DRC kumeendelea kutokana na uwepo wa "nguvu hasi" kwenye eneo hilo, ambazo zimeendelea kuchochea hali ya kutoaminiana kati ya nchi za kanda hiyo, na kutishia amani na utulivu wa kikanda.

    Amesisitiza kuwa kuondoa nguvu hizo kunatakiwa kupewa kipaumbele katika juhudi za kutekeleza Makubaliano ya Amani, usalama na ushirikiano nchini DRC.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako