• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi nchini Tanzania waanza kumtafuta bilionea kijana aliyetekwa nyara

    (GMT+08:00) 2018-10-12 09:45:10

    Polisi wa Tanzania wameanza msako wa watu waliomteka nyara mfanyabiashara bilionea kijana, aliyetekwa nyara jana alfajiri mjini Dar es salaam, alipokuwa akielekea kufanya mazoezi. Mfanyabiashara huyo Mohammed Dewji alitekwa na watu wasiojulikana alipokuwa anashuka kwenye gari yake, kwenye eneo la Oysterbay.

    Kamanda wa polisi wa kanda wa maalum ya Dar es salaam Bw. Lazaro Mambosasa ametangaza kuanza kwa msako huo, na kutaka umma kuwa na utulivu wakati uchunguzi unaendelea, lakini amesema walinzi watatu wa jumba la mazoezi wanashikiliwa na polisi kwa uchunguzi.

    Sababu ya Mohammed Dewji kutekwa nyara bado hazijatajwa, lakini imefahamika kuwa alitekwa nyara na wageni wawili ambao utaifa wao haijajulikana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako