• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa mataifa wataka maendeleo ya wazi kwenye suala la mpaka kati ta Sudan na Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2018-10-12 09:45:31

    Baraza la usalama la umoja wa mataifa limeamua kurefusha muda wa tume ya ulinzi wa amani ya umoja huo kwenye eneo la mpaka la Abyei linalogombewa na Sudan na Sudan Kusini kwa mara ya mwisho, isipokuwa kama kutakuwa na maendeleo yanayopimika kwenye suala hilo.

    Azimio namba 2438 lililopitishwa kwa kauli moja na baraza la usalama, limerefusha mamlaka ya tume hiyo hadi Aprili 15 mwaka kesho, hadi nchi hizo mbili zitakapoweza kuonyesha mpaka ili tume hiyo isiendelee kuwepo huko.

    Kupitia idhini hiyo baraza pia limeamua kupunguza idadi ya walinzi wa amani kufikia 4,500 hadi Novemba 15 mwaka huu, na kufikia 3,959 hadi Aprili 15 mwaka kesho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako