• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mfumuko wa bei nchini Sudan kwa mwezi Septemba ulipanda na kufikia asilimia 68

    (GMT+08:00) 2018-10-12 09:45:53

    Idara ya takwimu ya Sudan imetangaza kuwa mfumuko wa bei kwa mwezi septemba nchini Sudan ulipanda kutoka asilimia 66.82 na kufikia asilimia 68.64. Mfumuko huo umeonekana zaidi kwenye bei za chakula na vinywaji.

    Wiki iliyopita serikali ya Sudan ilitangaza hatua kadhaa za kiuchumi zinazohusu sekta za uuzaji na uagizaji wa bidhaa, ikiwa ni pamoja na kuweka kiwango kipya cha ubadilishaji wa dola ya Marekani kwa paundi kuwa 47.5, na kupunguza thamani yake kwa asilimia 63.8.

    Kufyatua hatua hizo, kumekuwa na upungufu mkubwa wa fedha taslimu kwenye mzunguko wa fedha, na kuzilazimu benki kufanya kazi leo ambayo ni siku ya mapumziko, ili kuweka fedha kwenye mashine za ATM.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako