• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika waipongeza Ethiopia kwa kurahisisha visa kwa wasafiri wa Afrika

    (GMT+08:00) 2018-10-12 10:09:08

    Umoja wa Afrika umeipongeza Ethiopia kwa kurahisisha upatikanaji wa visa kwa wasafiri kutoka nchi za Afrika.

    Rais Mulatu Teshome wa Ethiopia akihutubia mkutano wa bunge la umma Jumatatu wiki hii, alitangaza kuwa kuanzia mwaka wa fedha wa 2018/19, watu wenye pasipoti za nchi za Afrika watapewa visa ya Ethiopia moja kwa moja baada ya kuwasili katika nchi hiyo.

    Mwenyekiti wa baraza la Umoja wa Afrika Bw Moussa Faki Mahamat ameipongeza hatua hiyo, na kuitaja kuwa ni kitendo kinachoashiria nchi za Afrika zimeanza kuchukua hatua kurahishisha usafiri wa watu wa Afrika barani humo. Pia amehimiza nchi nyingine wanachama wa umoja huo zichukue hatua kama hiyo haraka iwezekanavyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako