• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri

    (GMT+08:00) 2018-10-12 10:09:28

    Katibu Mkuu wa ofisi ya waziri mkuu ya Ethiopia Bw Fitsum Arega, amesema Ethiopia inapanga kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri kutoka mawaziri 28 hadi 20 kwenye mchakato wa mageuzi ya serikali.

    Katika taarifa Bw. Arega amesema mpango wa kupunguza idadi ya taasisi za serikali unalingana na mpango wa kuungaisha nyadhifa za mawaziri na kuunda nyadhifa mpya, ambao ni kipaumbele kwa kazi za serikali kwa mwaka wa fedha wa 2018/19.

    Ameongeza kuwa hatua ya kupunguza ukubwa wa serikali ni kwa ajili ya kubana matumizi, kuhakikisha kazi za taasisi za serikali zinafanyika kwa ufanisi, na kuondoa taasisi zinazofanana katika serikali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako