• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bibi Peng Liyuan atoa pongezi hafla ya kutoa tuzo ya elimu ya wanawake na wasichana UNESCO

    (GMT+08:00) 2018-10-12 10:09:56

    Hafla ya kutoa tuzo ya tatu ya elimu ya wanawake na wasichana iliyoandaliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO imefanyika jana mjini Paris, Ufaransa. Mke wa rais Xi Jinping wa China Bibi Peng Liyuan akiwa ni mjumbe maalumu wa kuhimiza elimu ya wanawake na wasichana wa UNESCO ametoa salamu za pongezi kwenye hafla hiyo.

    Bibi Peng Liyuan amesema kazi ya kutoa elimu kwa wanawake na watoto wa kike ni kazi ya kifahari. Kuendeleza elimu kwa wanawake na watoto wa kike na kuwapatia usawa wa nafasi ya kujiendeleza ni muhimu katika kutimiza lengo la maendeleo endelevu kuelekea mwaka 2030.

    Ameongeza kuwa tuzo hiyo ni kwa ajili ya kuwahamasisha watu wengi zaidi kushiriki kwenye kazi hiyo ya kuhimiza usawa wa kupata elimu na kuwasaidia wanawake na watoto wa kike kutimiza ndoto zao. Amesema anapenda kuiunga mkono UNESCO katika kuhimiza mambo ya usawa wa kijinsia duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako