• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China haina nia ya kuingilia mambo ya ndani ya Marekani

    (GMT+08:00) 2018-10-12 10:19:01

    China imesema haina nia ya kuingilia mambo ya ndani ya Marekani, na hatua inazochukua dhidi ya Marekani ni za kimantiki na kujizuia, kwa lengo la kulinda maslahi yake na utaratibu wa biashara ya pande nyingi.

    Hayo yamesemwa na msemaji wa Wizara ya Biashara ya China Bw. Gao Feng, baada ya Marekani kusema vitendo vya China katika kutatua mgogoro wa kibiashara na Marekani vinashukiwa kuingilia mambo ya ndani ya Marekani, na China inajaribu kuwaathiri viongozi wa biashara wa Marekani kwa njia ya kuwatishia. Bw. Gao amesisitiza kuwa Marekani ndio inazusha mgogoro wa kibiashara na China, na kwamba dhamira ya China ya kulinda maslahi yake hahali haibadiliki, na nia yake ya kulinda maendeleo ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati yake na Marekani pia haijabadilika.

    Bw. Gao ameongeza kuwa China inakaribisha makampuni na wawekezaji wa Marekani na kuamini kuwa watafanya chaguo kwa usahihi.

    Kuhusu kauli iliyotolewa na upande wa Marekani inayosema kuwa itachukua hatua kali zaidi ili kuilazimisha China ifungue zaidi mlango wake, Bw. Gao amesema umwamba wa Marekani na vitendo vyake vya kuishinikiza China havisaidii kitu hata kidogo, na kwa ujumla uchumi wa China unaendelea vizuri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako