• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya watu waliofariki kutokana na maporomoko ya udongo nchini Uganda yafikia 35

    (GMT+08:00) 2018-10-12 16:49:16

    Polisi nchini Uganda imesema idadi ya watu waliofariki kutokana na maporomoko ya udongo mashariki mwa nchi hiyo yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha jana kwenye wilaya ya Bududa, mkoani Elgon imefikia 35 na wengine zaidi ya 30 wamejeruhiwa.

    Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Uganda limesema watu walikumbwa na hofu na kukimbia makazi yao wakati mvua kubwa ikiendelea kunyesha kwenye mkoa huo.

    Rais Yoweri Museveni wa nchi hiyo amewataka wakazi wa maeneo yaliyoathiriwa zaidi kushirikiana na mamlaka za huko ili kuepuka hatari zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako