• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Thamani ya jumla ya uagizaji na uuzaji wa bidhaa nje ya China katika robo tatu ya mwaka huu yaongezeka kwa asilimia 9.9

    (GMT+08:00) 2018-10-12 18:36:09

    Takwimu zilizotolewa na Idara Kuu ya Forodha ya China zinaonesha kuwa, katika robo tatu ya mwaka huu, thamani ya jumla ya uagizaji na uuzaji wa bidhaa nje ya China iliongezeka kwa asilimia 9.9 kuliko mwaka jana wakati kama huu.

    Msemaji wa Idara kuu ya Forodha ya China Bw. Li Kuiwen amesema, katika robo ya tatu ya mwaka huu, hali ya jumla ya biashara ya nje ya China ilipata maendeleo kwa hatua madhubuti. Anasema:

    "Katika kipindi hicho, thamani ya uuzaji wa bidhaa nje ya China katika Umoja wa Ulaya, Marekani, na Umoja wa Nchi za Asia Kusini Mashariki ASEAN iliongezeka kwa asilimia 7.3, asilimia 6.5 na asilimia 12.6 mtawalia, na thamani ya jumla inachukua asilimia 41.2 ya ile ya jumla ya uagizaji na uuzaji wa bidhaa nje ya China. Wakati huo huo, thamani ya uagizaji na uuzaji wa bidhaa ya China katika nchi zinazojiunga na "Ukanda Mmoja, Njia Moja" zikiwemo Russia, Poland, Kazakhstan iliongezeka kwa asilimia 19.4, asilimia 11.9 na asilimia 11.8 mtawalia, ambayo inazidi ile ya wastani."

    Takwimu hizo pia zimeonesha kuwa, thamani ya uagizaji na uuzaji wa bidhaa nje ya China nchini Marekani imefikia dola bilioni 443.5 za kimarekani, ambayo inachukua asilimia 13.8 ya thamani ya jumla ya biashara ya nje ya China, na Marekani inaendelea kuwa mwenzi wa pili wa biashara wa China. Bw. Li Kuiwen amesema, mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani umeleta usumbufu na athari kwa maendeleo ya biashara ya nje ya China lakini unaweza kudhibitiwa, anasema:

    "Kwa ujumla biashara kati ya China na Marekani ni ya kunufaishana. China ina mnyororo kamili wa viwanda na uwezo mkubwa wa utengenezaji, huku soko la Marekani linategemea sana bidhaa zinazotengenezwa China."

    Bw. Li Kuiwen pia emeeleza kuwa, tokea mwaka huu uanze, thamani ya uagizaji na uuzaji wa bidhaa nje wa China inapata ongezeko la kasi, huku ubora na ufanisi wa maendeleo ukizidi kuinuka. Pia ameeleza kuwa ongezeko la kasi la thamani ya uagizaji na uuzaji bidhaa wa nje, limeweka msingi imara kwa maendeleo yenye utulivu wa biashara ya nje kwa mwaka mzima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako