• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya China yashiriki katika jaribio la kudhibiti jangwa nchini Morocco

    (GMT+08:00) 2018-10-12 18:42:07

    Kampuni ya China Elion Group imesaini Makubaliano ya Awali na serikali ya Morocco yenye lengo la kudhibiti kuenea kwa jangwa katika mkoa wa Oriental nchini humo.

    Mwenyekiti wa kampuni hiyo Wang Wenbiao amesema, kampuni yake imepata uzoefu wa kuzuia na kudhibiti kuenea kwa jangwa katika miaka 30 ya kusimamia jangwa la Kubuqi kwenye mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani nchini China. Amesema Morocco ni nchi ya kwanza kutumia mfumo wa ikolojia wa kampuni ya Elion barani Afrika.

    Naye rais wa Baraza la Mkoa wa Oriental nchini Morocco Abdenbi Bioui amesema, kundi la Elion lina uzoefu mkubwa katika kusimamia jangwa la Kubuqi, hivyo kuleta matumaini mapya ya kuzuia na kudhibiti kuenea kwa jangwa katika mkoa wa Oriental.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako