• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hatua za biashara za Marekani zaharibu utaratibu wa biashara wa ulimwengu

    (GMT+08:00) 2018-10-12 19:21:29

    Shirika la Fedha la Kimataifa IMF hivi karibuni limetoa ripoti mpya ikipunguza kadirio la ukuaji wa uchumi wa dunia kwa mwaka huu na ujao kutoka asilimia 3.9 ya mwezi wa Aprili hadi asilimia 3.7. Shirika hilo limesema, katika mazingira yenye sera isiyo na uhakika, hatari ya biashara imekuwa changamoto kubwa inayoukabili uchumi wa dunia.

    Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Bibi Christine Lagarde amewahimiza viongozi wa nchi mbalimbali kushikana mikono kurekebisha mfumo wa biashara wa dunia badala ya kuuharibu.

    Siku kadhaa zilizopita, makamu wa rais wa Marekani Bw. Mike Pence alitoa hotuba ambapo alisema, rais Trump ameweka bayana kuwa, China na Marekani zinatakiwa kufikia makubaliano ya usawa na kunufaishana, la sivyo ushuru zaidi utatozwa dhidi ya bidhaa za China.

    Hivyo ni dhahiri kwamba Marekani imekuwa chanzo cha sera isiyo na uhakika, mtengenezaji wa hatari za biashara, na nchi inayoharibu mfumo wa biashara wa dunia. Lakini katika hotuba yake, Bw. Pence amesema kuwa, kitendo cha kuleta vita vya kibiashara vya dunia kinatokana na rais Trump kuiongoza Marekani kulinda maslahi yake kupitia nguvu yake. Kitendo ambacho Marekani inadai kufanya mazungumzo ili kufikia makubaliano huku ikitumia fimbo ya kuongeza ushuru kimechukuliwa kama hatua ya lazima ya "Marekani Kwanza".

    Tangu serikali ya Marekani ya awamu hii iingie madarakani, imechukua hatua ya kujinufaisha, kujilinda kibiashara na upande mmoja, huku ikiharibu uaminifu wake wa kitaifa na moyo wa mkataba. Ikulu ya Marekani imesema mara nyingi kuwa imetoa fursa nyingi kwa China kuichukulia Marekani kwa njia ya usawa zaidi, lakini China haitaki kubadilisha hatua yake. Ukweli ni kwamba China imetoa fursa nyingi kwa Marekani kurekebisha makosa yake ya kuanzisha vita vya kibiashara, na kuonesha nia safi ya kutatua mivutano ya kibiashara kupitia mazungumzo. Kwa bahati mbaya, Marekani imepoteza uaminifu na fursa mara kwa mara. Kupitia hotuba ya Bw. Pence, tunaweza kuona kwamba Marekani haitaki kutatua suala hilo, inataka kutumia hatua yake kutimiza nchi hiyoiwe na nguvu kubwa zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako