• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Airtel Tanzania yatangaza kutoa gawio la Sh1.4 bilioni kwa wateja wake

  (GMT+08:00) 2018-10-12 20:33:25

  Kampuni ya Airtel Tanzania imetangaza kutoa gawio la shilingi bilioni 1.4 kwa wateja wake wa huduma ya Airtel Money. Mkurugenzi wa masoko na Airtel Money, Isack Nchunda amesema gawio hilo litatolewa kwa wateja wote pamoja na mawakala wa Airtel Money waliotumia huduma hiyo kwa miezi mitatu ya kwanza mwaka huu yaani Januari hadi Machi.

  Gawio hilo hutolewa katika kila robo ya mwaka tangu mwaka 2015. Mpaka Machi, takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinaonyesha Airtel Money ilikuwa na wateja milioni 3,923 ambao waliongezeka mpaka milioni 4.07 Juni na kuiweka nafasi ya tatu ikitanguliwa na M-Pesa ilikuwa nao milioni 8.642 na Tigo Pesa milioni 6.979.

  Meneja wa Airtel Money, Ibrahim Malando amesema kuanzia sasa kila mteja au mawakala wa Airtel Money atapokea gawio kupitia akaunti yake ya Airtel Money.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako