• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jumuiya ya SCO yatoa taarifa ya pamoja na kupinga kujilinda kibiashara

    (GMT+08:00) 2018-10-13 16:59:06

    Mkutano wa 17 wa bodi ya wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya ushirikiano ya Shanghai SCO umefungwa jana huko Dushanbe nchini Tajikstan. Taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya mkutano huo imesisitiza kuwa, nchi wanachama wa jumuiya ya SCO zitaimarisha mfumo wa biashara unaoshirikisha pande nyingi, kupinga aina yoyote ya kujilinda kibiashara. Hii ni mara nyingine kwa jumuiya hiyo kutoa sauti ya pamoja kuhusu kulinda mfumo wa pande nyingi na biashara huria.

    Kwenye kipindi cha mkutano huo, wakuu wengi akiwemo waziri mkuu wa Russia Bw. Dimitri Medvedev walilaani vitendo vya nchi fulani kuhusu kujilinda kibiashara, kuweka vikwazo dhidi ya nchi nyingine peke yake, na kutishia kisiasa. Hii imeonyesha kuwa jumuiya ya SCO inaonesha umuhimu mkubwa zaidi katika kupinga kujilinda kibiashara na kulinda mfumo wa pande nyingi.

    Kwenye mkutano huo, waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ametoa pendekezo la kuzindua utafiti wa uwezekano wa kuanzisha eneo la biashara huria la jumuiya ya SCO, na kupanga hatua kwa hatua mpango wa utaratibu wa ushirikiano wa kikanda. Taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya mkutano huo pia imetangaza kuwa, pande mbalimbali zimetetea kuhimiza urahisi wa biashara na uwekezaji, ili kutimiza hatua kwa hatua mawasiliano huria ya bidhaa, mitaji, huduma na teknolojia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako