• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bw. Li Keqiang ahudhuria mkutano wa 17 wa baraza la viongozi wa serikali za nchi wanachama wa shirika la ushirikiano la Shanghai

    (GMT+08:00) 2018-10-13 17:03:02

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang jana alasiri huko Dushanbe alihudhuria mkutano wa 17 wa baraza la viongozi wa serikali ya nchi wanachama wa shirika la ushirikiano la Shanghai. Waziri mkuu wa Tajikistan Bw. Kokhir Rasulzoda, waziri mkuu wa Russia Bw. Dimitri Medvedev, waziri mkuu wa Kazakhastan Bw. Bakytzhan Sagintayev, waziri mkuu wa Kyrgyzstan Bw. Mukhammedkaliy Abylgaziyev, waziri mkuu wa Uzbekisan Bw. Abdulla Aripov na wajumbe kutoka Pakistan, India na nchi za wachunguzi walihudhuria mkutano huo.

    Bw. Li Keqiang alisema kuwa katika miaka 17 iliyopita tangu kuundwa kwa shirika hilo, shirika hilo limepata mafanikio na kutoa mchango kwa kulinda amani na utulivu wa bara la Asia na bara la Ulaya na kuhimiza maendeleo na ustawi wa eneo hilo. Bw. Li alisisitiza kuwa mwaka huu ni miaka ya 40 ya kufanya mageuzi na kufungua mlango kwa nchi za nje kwa China. Shirika hilo ni jukwaa muhimu la ujenzi wa Ukanda moja na Njia moja na linapaswa kuwa mfano wa kufanya ushirikiano na kupata maendeleo kwa pamoja kwa nchi za eneo hilo.

    Bw. Li Keqiang alisaini na kutangaza taarifa ya pamoja na kuidhinisha maazimio na makubaliano katika sekta ya uchumi, biashara, sayansi na teknolojia pamoja na uhifadhi wa mazingira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako