• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya Utunzaji mazingira ya China yatafuta fursa ya kuendeleza mazingira nchini Nigeria

    (GMT+08:00) 2018-10-14 16:21:02

    Kampuni ya China inayojihusisha na utunzaji wa mazingira iitwayo ERG jana imesaini mkataba wa makubaliano na serikali ya jimbo la Kusini mwa Nigeria la Imo ikiwa ni sehemu ya kutafuta fursa za uwekezaji nchini humo, hasa katika kukabiliana na kudhibiti ongezeko la ukame na hali ya jangwa, kilimo na maendeleo ya vyanzo vipya vya nishati.

    Kiongozi wa ERG ambaye aliongoza ujumbe wa kampuni kusaini makubaliano hayo Wang Wenbiao, alieleza utayari wa kampuni yake kusaidia matumizi sahihi ya maliasili ya gesi iliyopo eneo hilo ili kuongeza uzalishaji wa nishati kwa ajili ya matumizi ya majumbani na matumizi ya viwandani.

    Aidha Bw. Wang alisema utafutaji wa fursa nchini Nigeria unatokana na mafanikio ya mkutano wa wakuu wa nchi za China na Afrika uliofanyika mjini Beijing mwezi uliopita, ambapo China ilipendekeza uendelezaji wa hali ya kijani kama moja ya mapendekezo 8 iliyotangaza ili kuimarisha na kukuza ushirikiano na Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako