• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka, Mechi za kufuzu AFCON 2019: Kenya, Uganda zapata ushindi

  (GMT+08:00) 2018-10-15 08:45:06

  Timu ya taifa ya soka ya Kenya imefanikiwa kupata na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Ethiopia na kuongoza kundi lake la kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika AFCON mwakani nchini Cameroon.

  Magoli ya Kenya katika mechi hiyo yalifungwa na Michael Olunga, Eric Johana na Victor Wanyama aliyefunga kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 67.

  Kenya inafikisha alama saba baada ya kucheza mechi nne F ambalo pia lina timu za Ghana na Sierra Leone.

  Kwa upande wa timu zingine za Afrika Mashariki Uganda ilishinda mechi yake ya ijumaa kwa magoli 3-0 dhidi ya Lesotho na sasa inaongoza kundi L, Tanzania ikafungwa Cape Verde kwa magoli 3-0.

  Rwanda inashika nafasi ya mwisho kwenye H ikiwa haina alama hata moja baada ya kufungwa mechi zote tatu mpaka sasa, na Burundi ikiwa katika nafasi ya pili kwa kuwa na alama tano katika kundi C.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako