• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanafunzi wa Ethiopia wahimizwa kujizuia na "ajenda za hujuma"

    (GMT+08:00) 2018-10-15 09:32:36

    Serikali ya Ethiopia imewahimiza wanafunzi wa elimu ya juu kote nchini kujizuia na aina yoyote ya "ajenda za hujuma", na kufanya maamuzi yenye mantiki wakati wanapoingia kwenye muhula mpya wa masomo.

    Wito huo umetolewa na waziri mkuu wa Ethiopia Bw. Abiy Ahmed na naibu wake Bw. Demeke Mekonnen. Bw. Ahmed pia amewataja wanafunzi kuwa na mustakbali wa nchi yao, na kuwashauri kujitahidi kadiri wawezavyo kutokana na ajenda za kitaifa, ili kuweza kuchangia maendeleo ya nchi yao.

    Vyuo vikuu nchini Ethiopia vilikuwa ni chanzo kikuu cha vurugu zilizotokea hivi karibuni na kuiathiri nchi nzima tangu nusu ya pili ya mwaka 2016, kutokana na changamoto zinazohusiana na ufisadi na utawala mbaya. Takwimu zilizotolewa na serikali ya Ethiopia zinaonesha kuwa zaidi ya asilimia 70 ya wananchi wake ni vijana walio chini ya miaka 30.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako