• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Somalia yatoa mwito wa kuwepo kwa umoja wakati ikikumbuka mauaji ya mwezi Oktoba

    (GMT+08:00) 2018-10-15 09:48:25

    Jumuiya ya kimataifa jana iliungana na Somalia kwenye maombolezo ya vifo vya watu 587 na wengine 316 waliojeruhiwa kwenye shambulizi la bomu lililotokea Oktoba 14 mwaka 2017. Wabunge na maofisa wa serikali ya Somalia wametumia siku hiyo kutoa mwito wa kuwepo kwa umoja, amani na masikilizano, vitakavyosaidia kuleta amani ya kudumu nchini Somalia.

    Akiongea kwenye mkusanyiko wa kuwakumbuka watu hao uliofanyika kwenye makutano ya barabara ya Zoope, ulipotokea mlipuko huo, Waziri Mkuu wa Somalia Bw. Hassan Khaire, amesema tukio hilo la kigaidi ni tukio kubwa zaidi katika historia ya Somalia.

    Waziri Mkuu huyo pia amesema mamia ya wasomali wanaendelea kuteseka na madhara ya kimwili na kisaikolojia yaliyotokana na shambulizi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako