• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la katiba la Cameroon kusikiliza ombi la kutaka matokeo ya uchaguzi wa rais yabatilishwe

    (GMT+08:00) 2018-10-15 09:48:45

    Baraza la katiba la Cameroon kesho litaanza kusikiliza ombi kutoka kwa baadhi wagombea wa upinzani na wapiga kura wanaotaka matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika Oktoba 7 yabatilishwe.

    Jumla ya mazuio 25 yamewasilishwa kwa tume ya uchaguzi ya Cameroon yakitaka sehemu ya matokeo ya uchaguzi, au matokeo yote ya uchaguzi yabatilishwe. Wagombea watatu wa urais wamelalamikia mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na "ukiukaji wa taratibu" na "kutoheshimu sheria ya uchaguzi", kulikoonekana wakati wa upigaji kura.

    Ijumaa iliyopita mwenyekiti wa tume ya uchaguzi alitoa mwito wa kuwepo kwa utulivu wakati nchi ikisubiri matokeo ya mwisho ya uchaguzi. Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi ya Cameroon, Baraza la katiba litatangaza matokeo ya mwisho ya uchaguzi Oktoba 22.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako