• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa Uturuki na Saudi Arabia wafanya mazungumzo kuhusu mwandishi wa habari aliyepotea

    (GMT+08:00) 2018-10-15 09:49:09

    Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki jana alifanya mazungumzo na mfalme Salman Abdulaziz, kuhusu mwandishi wa Saudi Arabia Jamal Kashoggi aliyepotea tangu oktoba 2 alipoingia kwenye ofisi ya ubalozi wa Saudi Arabia nchini Uturuki.

    Kwenye maongezi kati yao viongozi hao wawili wamesisitiza umuhimu wa kuunda kikundi cha pamoja kufanya uchunguzi kuhusu tukio hilo.

    Baada ya maongezi yao wizara ya mambo ya nje ya Saudi Arabia ilitoa tweet inayosema, Mfalme wa Saudi Arabia amesisitiza uimara wa uhusiano kati ya Saudi Arabia na Uturuki, na kusema hakuna anayeweza kuyumbisha uhusiano huo.

    Habari zisizothibitishwa zinasema mwanahabari wa gazeti la Washington Post Bw. Jamal Kashoggi inawezekana aliuawa ndani ya ofisi ya ubalozi wa Saudi Arabia mjini Istanbul, lakini maofisa wa Saudi Arabia wamekanusha madai hayo na kusema kuwa "hayana msingi".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako