• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Algeria inapenda kuendeleza ushirikiano wa kunufaishana na Nigeria

    (GMT+08:00) 2018-10-15 09:55:42

    Waziri wa mambo ya nje wa Algeria Bw. Abdelkader Messahel amesema Algeria inapenda kuendeleza ushirikiano na Nigeria ulio wa kunufaisha pande mbili.

    Katika mkutano wa nne wa tume ya pamoja ya ngazi ya juu kati ya Algeria na Nigeria uliofanyika mjini Algiers, Bw Messahel amesema dhamira iliyozihimiza nchi hizo mbili kuwa na ushirikiano, inatakiwa kuonekana kwenye utekelezaji wa miradi halisi kwa msingi wa fursa zilizopo na kusaidiana.

    Bw. Messahel ameongeza kuwa tume hiyo ambayo yeye na mwenzake wa Nigeria Bw Geoffrey Onyeama ni wenyekiti wenza, itakuwa sehemu muhimu ya mchakato wa kuanzisha ushirikiano mpya wenye mafanikio kati ya nchi zote mbili, na makubaliano kadhaa ya ushirikiano yatasainiwa kwenye mkutano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako