• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yalazimisha nchi nyingine zisifikie makubaliano ya biashara na China

    (GMT+08:00) 2018-10-15 16:53:03

    Marekani hivi karibuni ilifikia makubaliano ya biashara na Mexico na Canada USMCA. Kwa mujibu wa kipengele cha 32 cha USMCA, nchi yoyote ikifikia makubaliano ya biashara na nchi zenye uchumi usio wa soko huria, nchi nyingine mbili zitajitoa kwenye USMCA ndani ya miezi 6. Kipengele hicho kinaaminika kuilenga China. Gazeti la Financial Times la Uingereza limetoa ripoti ikisema, vipengele vingi vya USMCA vinalenga kuzuia maendeleo ya China, na kuhakikisha Canada na Mexico pia zinafanya hivyo.

    Waziri wa biashara wa Marekani Bw Wilbur Ross alikiita kipengele cha 32 cha USMCA "dawa ya sumu", na kusema Marekani itajitahidi kuweka kipengele hicho kwenye makubaliano ya biashara na nchi nyingine zikiwemo Japan, Uingereza na nchi za Umoja wa Ulaya. Je, Marekani itafanikiwa kulazimisha nchi nyingine kunywa "dawa" hiyo, na kujenga mfumo wa biashara dhidi ya China duniani?

    Kwanza, Canada haifurahii "dawa" hiyo. Kuhusu USMCA, mwenyekiti wa shirikisho la wafanyabiashara la Canada Bw. Perrin Beatty amesema, Canada inapaswa kukumbuka fundisho hilo, na isitegemee soko moja tu baadaye. Naye waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Bibi Chrystia Freeland alipokutana na mwenzake wa China Bw. Wang Yi amesema, Canada itajiamulia kusukuma mbele mazungumzo ya biashara huria na nchi nyingine, kupenda kuongeza uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati yake na China, na kuongeza mawasiliano na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta mbalimbali.

    Pili, ni vigumu kwa Marekani kuzilazimisha nchi nyingine kupokea "dawa hiyo ya sumu". China ni soko kubwa zaidi la bidhaa za Japan, na kushika nafasi ya kwanza duniani kwa ukubwa wa biashara wa nje wa Japan. Hivyo Japan haiwezi kuacha kufanya biashara na China kutokana na matakwa ya Marekani. Kwa upande wa Umoja wa Ulaya, baada ya Marekani kujitoa kwenye makubaliano ya suala la nyuklia la Iran, umoja huo umejenga shirika maalumu la kudumisha biashara na Iran kwa kushirikiana na Russia na China, ili kuepuka vikwazo vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Iran. Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa hivi karibuni alitangaza kwenye Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kuwa, nchi yake haitafikia makubaliano ya biashara na nchi zisizoheshimu makubaliano ya Paris kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa. Marekani ni nchi pekee iliyojitoa kwenye makubaliano hayo. Hivyo Umoja wa Ulaya pia hauwezi kupokea "dawa ya sumu" ya Marekani.

    Tatu, China inabadilisha njia yake ya kuendeleza uchumi, na matumizi ya ndani yatakuwa nguzo kubwa zaidi ya maendeleo ya uchumi badala ya biashara ya nje. Inakadiriwa kuwa mwaka huu thamani ya matumizi nchini China itakuwa sawa au kuzidi thamani hiyo ya Marekani. Wakati huo huo, China bado ni nchi ya kwanza kwa ukubwa wa biashara kwa nchi zaidi ya 120 duniani. Marekani haitaweza kuzuia maendeleo ya China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako