• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu wa Cameroon yawasilishwa kwenye Baraza la katiba

    (GMT+08:00) 2018-10-16 09:00:51

    Kamisheni ya kuhesabu kura ya Cameroon imewasilisha matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 7 kwenye Baraza la katiba la nchi hiyo.

    Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi ya Cameroon, baraza la katiba linatarajiwa kuamua na kutangaza matokeo ya uchaguzi ndani ya siku 15 baada ya kumalizika kwa upigaji kura, na maamuzi yatakayotolewa na baraza hilo yatakuwa ni ya mwisho.

    Katibu mkuu wa baraza hilo Bw. Malego Joseph Asse amesema kupitia taarifa kuwa, leo baraza lake litaanza kusikiliza maombi ya pingamizi ya wagombea wa upinzani kutaka matokeo ya uchaguzi yabatilishwe kutokana na tuhuma za ukiukaji kanuni za uchaguzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako