• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu ya Uturuki yaingia kwenye ubalozi wa Saudi Arabia mjini Istanbul kutafuta mwanahabari aliyepotea

    (GMT+08:00) 2018-10-16 09:01:15

    Ujumbe wa Uturuki umeingia kwenye ubalozi wa Saudi Arabia mjini Istanbul kumtafuta mwanahabari wa Saudi Arabia aliyepotea Bw. Jamal Khashoggi.

    Ujumbe huo unaoshirikisha maofisa wa polisi na wapelelezi wa matukio ya uhalifu CSI, uliingia kwenye ubalozi wa Saudi Arabia jana usiku, na polisi wameimarisha hatua za usalama kwenye eneo la karibu na kufunga barabara zinazoelekea kwenye ubalozi huo.

    Wiki iliyopita Uturuki na Saudi Arabia zilifikia makubaliano ya kushirikiana kwenye tukio hilo na kufanya utafutaji wa pamoja kwenye ubalozi huo, ambako Bw. Khashoggi alionekana mara ya mwisho Oktoba 2. Uturuki inaamini kuwa mwanahabari huyo ameuawa na mwili wake umeondolewa, huku Saudi Arabia ikikanusha tuhuma hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako