• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Afrika Kusini akanusha kushindwa kuchukua hatua kuhusu kashfa ya Benki

    (GMT+08:00) 2018-10-16 09:19:30

    Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amekanusha ripoti za vyombo vya habari, kuwa amepuuza kuchukua hatua dhidi ya benki moja nchini Afrika ya Kusini inayotuhumiwa kwa ukiukaji wa taratibu za kifedha.

    Msemaji wa Rais Bw. Khusela Diko, amesema Rais Ramaphosa hakumbuki kama kulikuwa na mkutano wowote kati yake na mtu yeyote mwenye uhusiano na benki ya VBS Mutual, huku akiwa na taarifa kama hizo.

    Gazeti la City Press limeripoti kuwa Rais Ramaphosa alifahamu kuhusu uporaji katika benki hiyo lakini hukuchukua hatua yoyote.

    Ripoti iliyotolewa wiki iliyopita, imesema Benki Kuu ya Afrika Kusini imewataja watu 50 wenye uhusiano na vyama vya ANC na EFF, wanaotuhumiwa kutumia ushawishi wao wa kisiasa kupora na kukiuka taratibu za kifedha za benki hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako