• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa biashara wa Afrika kukutana Kenya kuhimiza biashara ya ndani ya Afrika

    (GMT+08:00) 2018-10-16 09:19:52

    Chama wa wafanyabiashara na wanaviwanda wa Kenya wiki ijayo kitaandaa mkutano wa pili utakaowakutanisha viongozi wa biashara kutoka nchi mbalimbali za Afrika, kutafuta njia za kuhimiza biashara ya ndani ya Afrika.

    Chama hicho kimetangaza kuwa mkutano huo utafanyika kati ya Oktoba 23 na 24, ukiwa na lengo kuharakisha makubaliano ya biashara huria ya Afrika, pamoja na kujiandaa kwa jumuiya ya wafanyabiashara wa Afrika.

    Mwenyekiti wa chama hicho Bw. Kiprono Kittony, ambaye pia ni makamu mwenyekiti cha Shirikisho la wafanyabiashara duniani, amesema mkutano huo unatarajiwa kufanyika katika wakati mzuri na sahihi, wakati nchi za Afrika zinajipanga kuondoa vizuizi vya biashara kati yao.

    Baadhi ya mambo yatakayojadiliwa kwenye mkutano huo ni pamoja na changamoto zinazovikabili vyama vya wafanyabiashara, namna ya kuvijenga vyama hivyo kuwa endelevu, na mchango wa vyama hivyo katika kuhimiza biashara ya ndani barani Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako