• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yafanya maonesho ya biashara ili kutangaza bidhaa zake

    (GMT+08:00) 2018-10-16 09:27:24

    Maonesho ya pili ya "Made in Sudan Kusini" yamefunguliwa jana huko Juba, mji mkuu wa nchi hiyo, yakiwa na lengo la kutangaza bidhaa zinazotengenezwa Sudan Kusini na kupanua fursa ya uwekezaji nchini humo.

    Waziri wa biashara, viwanda na mambo ya jumuiya ya Afrika Mashariki EAC wa Sudan Kusini Bw. Paul Akech, amesema maonesho ya mwaka huu yanaonesha uwezo wa kilimo na viwanda wa nchi hiyo, ili kupunguza utegemezi wa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje.

    Bw. Akech amesema serikali ya Sudan Kusini inajaribu kuhimiza maendeleo ya sekta ya viwanda nchini humo kupitia kutekeleza sheria za kuwalinda wawekezaji na wateja wa ndani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako