• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Algeria na Nigeria zakubaliana kuhimiza miradi mikubwa ya ushirikiano kati yao

    (GMT+08:00) 2018-10-16 09:27:51

    Algeria na Nigeria zimesema zimesaini makubaliano ya kuhimiza miradi mikubwa ya ushirikiano kati yao. Makubaliano hayo yamefikiwa wakati wa ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Nigeria Bw. Geoffrey Onyeama nchini Algeria.

    Kwa mujibu wa mpango uliosainiwa na waziri wa mambo ya nje wa Algeria Bw. Abdelkader Messahel na mwenzake wa Nigeria Bw. Onyeama kwenye mkutano wa nne wa kamati ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, ushirikiano huo unahusisha sekta za nishati, uchukuzi na mawasiliano.

    Bw. Messahel amesema mpango huo umefafanua hatua mbalimbali za utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na pande hizo mbili. Ameongeza kuwa nchi hizo mbili pia zitasaini makubaliano 10 ya ushirikiano kwenye sekta za biashara, viwanda, nishati na uwekezaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako