• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maofisa wa Kenya washitakiwa kutokana na vitendo vya ufisadi kwenye Michezo ya Olimpiki ya Rio

    (GMT+08:00) 2018-10-16 09:36:15

    Maofisa kadhaa wa Kenya wamefikishwa mahakamani kutokana na kutumia vibaya madaraka na kula pesa kwenye Michezo ya Olimpiki ya Rio. Maofisa hao akiwemo aliyekuwa katibu wa kudumu wa michezo wa Kenya mwaka 2016 wakati wa Michezo ya Olimpiki ya Rio Bw. Richard Ekai, katibu mkuu wa Kamati ya Olimpiki ya Kenya NOCK Bw Francis Kinyili na mkuu wa timu ya Kenya Bw. Stephen Soi walijitetea kuwa hawakutumia vibaya dola za kimarekani laki 5.4, pesa zilizotengwa kwa ajili ya Michezo hiyo. Maofisa wengine wawili Bw. Hassan Wario, balozi wa Kenya nchini Austria na aliyekuwa mwenyekiti wa NOCK walipewa muda mpaka Alhamisi ili kujisalimisha kwa polisi ili kuchunguzwa kuhusu kashfa za kifedha katika Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2016.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako