Mawaziri wa nishati wa Russia na Iran wamejadili hali ya soko la mafuta duniani na uwezekano wa kanuni kuhusu uzalishaji wa mafuta katika siku za baadaye, chini ya makubaliano yaliyofikiwa kati ya Shirika la Nchi Zinazozalisha Mafuta OPEC na wazalishaji wasio wa OPEC. Waziri wa nishati wa Russia Bw. Alexander Novak amesema kutokana na juhudi za pamoja, uzalishaji wa mafuta umeongezeka kwa mapipa milioni 1 kwa siku, na inatarajiwa kuwa nchi hizo mbili zitatuliza soko na kuwajibika katika kutengeneza kanuni tulivu na zinazotabiriwa katika sekta ya mafuta kwa ajili ya maslahi ya wazalishaji, wateja na wawekezaji wote.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |