• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Uholanzi zatoa wito wa kuhimiza biashara huria na kupinga kujilinda kibiashara

    (GMT+08:00) 2018-10-16 09:54:50

    China na Uholanzi zimetoa wito kwa nchi zote duniani kufanya juhudi za kuhimiza biashara huria na kulinda utaratibu wa dunia yenye ncha nyingi, ili kukabiliana na changamoto za pamoja zinazoikabili dunia.

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang na mwenzake wa Uholanzi Bw Mark Rutte jana walizungumza na wanahabari mijini The Hague, Bw Li Keqiang amesema nchi zote mbili zitaongeza juhudi za pamoja kuhimiza biashara huria na kuboresha zaidi mfumo wa biashara ya pande nyingi.

    Kwa upande wa utaratibu wa dunia yenye ncha nyingi, Bw Li Keqiang amesisitiza kwamba utartibu huo haumaanishi kutoheshimu uhusiano kati ya nchi, bali ni hatua ya kuhimiza demokrasia kwenye mambo ya siasa duniani. Amesisitiza tena dhamira ya China katika kuzidi kufungua mlango, na kusema China itapanua zaidi soko la uwekezaji kwa Uholanzi kwenye sekta za kilimo na huduma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako