• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Somalia lawaua wapiganaji 8 wa al-Shabab kusini mwa Somalia

    (GMT+08:00) 2018-10-16 09:55:11

    Jeshi la Somalia limepambana na wapiganaji wa Kundi la al-Shabab kusini mwa Somalia, na kuwaua wapiganaji wasiopungua wanane na kuwajeruhi wengine kadhaa.

    Kamanda wa divisheni ya 60 ya jeshi la Somalia Bw Ismail Khalif Shire amesema asakri mmoja aliuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa kwenye mapambano hayo yaliyotokea Daynunay, kilomita 30 mashariki mwa mji wa Baidoa.

    Bw. Shire amesema jeshi lake limewaua wapiganaji wanane wa Kundi la al-Shabab na kuwajeruhi wengine kadhaa, ambapo limevunja ndoto yao ya kutwaa eneo hilo. Wapiganaji wa Kundi la al-Shabab wamedai kuwa wamedhibiti eneo la Daynunay na kukamata silaha kutoka kituo cha jeshi kwenye eneo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako