• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yashika nafasi ya kwanza duniani katika kupokea uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje

    (GMT+08:00) 2018-10-16 18:39:30
    Ripoti iliyotolewa na Baraza la Biashara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa kuhusu usimamizi wa mwelekeo wa uwekezaji duniani imeonesha kuwa, katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje nchini China umeongeza kwa asilimia 6 na kufikia dola za kimarekani bilioni 70.

    Ripoti hiyo imesema, katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, kutokana na athari ya sera ya kodi ya Marekani, thamani ya uwekezaji wa moja kwa moja wa nchi za nje duniani ni dola za kimarekani bilioni 470 ambayo imepunguza kwa asilimia 41, ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu. Mkurugenzi wa idara inayoshugulikia uwekezaji na masuala ya makampuni ya baraza hilo Bw. Zhan Xiaoning amesema, China imeongeza nguvu ya kuvutia uwekezaji wa nje na kuendelea kufungua soko la ndani, na hivi sasa, China imekuwa nchi ya kwanza duniani katika kupokea uwekezaji huo.

    Habari nyingine kutoka idara ya takwimu ya China imesema, mwezi Septemba, mfumuko wa bei nchini China ilikuwaasilimia 2.5 na bei ya bidhaa za viwanda iliongeza kwa asilimia 3.6.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako