• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonesho ya 124 ya Canton Fair yafunguliwa mjini Guangzhou, China

    (GMT+08:00) 2018-10-16 18:42:01

    Maonesho ya 124 ya biashara na nje ya China yanayojulikana kama Canton Fair yamefunguliwa jana mjini Guangzhou, China. Makampuni ya China yamejitahidi kupanua soko la kimataifa kwa kuzingatia uvumbuzi.

    Maonesho hayo yenye vibanda 60,645 yameyashirikisha makampuni zaidi ya elfu 25 kutoka nchi na sehemu zaidi ya 210. Msemaji wa maonesho ya Canton Fair, ambaye pia ni naibu mkurugenzi wa kituo cha biashara na nje cha China Bw. Xu Bing amesema, maonesho ya awamu hii yamedumisha anuwai ya waagizaji. Anasema,

    "Maonesho hayo yametoa mchango chanya kwa makampuni, matoleo na chapa za China kujulikana duniani, kuihimiza China kubadilika kuwa nchi kubwa ya biashara, na maendeleo ya uchumi wa dunia kwa kufungua mlango."

    Hadi sasa maonesho ya Canton Fair yamesaini makubaliano ya ushirikiano na mashirika 46 ya viwanda na biashara ya nchi 32 zinazohusika na pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", ili kutoa huduma za habari, ushiriki wa maonesho na kuhamasisha biashara kwa ajili ya makampuni ya nchi hizo. Aidha, miongoni mwa nchi 10 zenye wafanyabiashara wengi zaidi wanaoshiriki kwenye maonesho hayo, nchi 7 zinahusika na pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja", zikiwemo India na Russia ambazo idadi ya wafanyabiashara wao wanaoshiriki kwenye maonesho ya Canton Fair imeongezeka kwa mfululizo. Msimamizi mkuu wa idara ya kimataifa ya Kampuni ya Vifaa vya Ujenzi ya Bode Bw. Li Rongjie amesema, kampuni hiyo inajitahidi kuboresha muundo wa matoleo, ili kupanua soko la kimataifa. Anasema,

    "Kusema kweli, katika soko la nchi za 'Ukanda Mmoja, Njia Moja', tunatetea zaidi matoleo yetu wenyewe. Licha ya hayo, pia tunashirikiana na makampuni mengine ili kuongeza uwezo wa ushindani katika soko la kimataifa."

    Huu ni mwaka wa 40 tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango. Katika miaka mingi iliyopita, maonesho ya Canton Fair yametoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya uchumi na biashara nchini China, kupitia hatua za mageuzi, uvumbuzi na kulinda haki miliki za ujuzi. Meneja mkuu wa idara inayoshughulikia mambo ya kimataifa ya Kampuni ya Sayansi na Teknolojia ya Kangmingsheng ya Shenzhen Bw. An Yuming anasema,

    "Licha ya maendeleo ya teknolojia ya mtandao wa Internet, tunaona kuwa maonesho ya Canton Fair bado ni jukwaa muhimu kwa makampuni ya uzalishaji viwandani kuonesha ubora wa makampuni, chapa na matoleo yao."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako