• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa asisitiza kuhimiza kazi ya kuondoa umaskini kwa pande zote

    (GMT+08:00) 2018-10-16 18:44:49

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesisitiza kuimarisha nguvu zaidi kwa maendeleo ya sayansi na teknolojia ili kuondoa umaskini na kutimiza lengo la kuondoa umaskini kabla ya mwaka 2030.

    Bw. Guterres amesema hayo katika taarifa yake kabla ya Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Umasikini ambayo huadhimishwa Oktoba 17 kila mwaka. Amesema katika miaka 25 iliyopita, chini ya kuhimiza maendeleo ya uchumi ya pande mbalimbali na ushirikiano wa kimataifa, watu bilioni 1 duniani wametoka kwenye umaskini. Lakini bado kuna watu zaidi milioni 700 wanaishi kwenye umaskini, hawawezi kunufaika katika maendeleo ya kasi ya uchumi wa dunia, na pia ni ngumu kupata fursa za matibabu, elimu na ajira. Hivyo inapaswa kuhimiza maendeleo yenye usawa zaidi duniani katika siku zijazo na kuongeza nguvu katikakutatua matatizo ya kijamii kwa watu wanaoishi kwenye umaskini uliokithiri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako