• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Afrika Kusini aahirisha ziara yake DRC kutokana na maradhi

    (GMT+08:00) 2018-10-16 18:50:39

    Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ameahirisha ziara yake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kutokana na maradhi katika mfumo wa kupitisha hewa.

    Msemaji wa ikulu ya nchi hiyo Khusa Diko amesema, rais Ramaphosa alitarajiwa kuwasili nchini DRC jana, lakini alishauriwa na madaktari kusubiri mpaka apone kabla ya kusafiri.

    Rais Ramaphosa na mwenzake Joseph Kabila wa DRC walitarajiwa kuridhia makubaliano yaliyofikiwa na nchi hizo mbili katika kikao cha 11 cha Tume ya Nchi hizo mbili kinachoendelea mjini Kinshasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako