• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ziara ya waziri mkuu wa China nchini Uholanzi yatoa alama muhimu ya nchi hizo mbili kuzidi kufungua mlango kwa upande mwingine

    (GMT+08:00) 2018-10-16 18:58:24

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang amesema, China inapenda kushirikiana na Uholanzi kuhimiza maendeleo ya uhusiano wa wenzi wa ushirikiano kwa pande zote kati ya nchi hizo mbili, ili kutoa mchango mkubwa zaidi katika kuhimiza amani, utulivu, maendeleo na ustawi wa dunia na wa kikanda.

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ambaye yuko ziarani nchini Uholanzi amefanya mazungumzo na viongozi wa Uholanzi na kushuhudia kusainiwa kwa makubaliano ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili.

    Bw. Lu amesema, pande hizo mbili zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta za jadi ikiwemo kilimo na nishati, na kupanua ushirikiano mpya katika utengenezaji wa bidhaa za kiwango cha juu na utoaji wa huduma. Bw. Li amesisitiza kuwa China inapenda kutoa mazingira ya biashara ya kisoko, kisheria na kimataifa kwa makampuni ya nchi mbalimbali, huku ikiendelea kushika sera ya mageuzi na ufunguaji mlango wazi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako