• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Wakaazi wa wilaya ya Lwengo walalamikia kukwama kwa mradi

    (GMT+08:00) 2018-10-16 19:27:16
    Wakaazi wa wilaya ya Lwengo nchini Uganda wamelalamikia miradi iliokwama ya unyunyiziaji mashamba maji ilioanzishwa miaka miwili iliopita.

    Miradi hiyo inatumia kawi ya miale ya jua na maji yake yanatoka kwenye eneo chepechepe la Kyoja.

    Hata hivyo familia 45 zilizolengwa kwenye mradi huo chini ya chama cha Kyassonko wanasema hawajafaidika kutokana na ukosefu wa maji.

    Msemaji wa baraza la wilaya ya Lwengo George Matovu Saitoti, amesema mipango imeanzisha ili kuweka vifaa vipya kwenye mfumo wa kusambaza maji ili kurejesha tena ukuzaji wa mboga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako