• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Wadau wa madini Rwanda waoba kuondolewa ada ya ufuatiliaji

    (GMT+08:00) 2018-10-16 19:27:33
    Wadau wa uchimbaji madini nchini Rwanda wameoba kuondolewa ada ya ufuatiliaji kabla ya kufanya uchimbaji.

    Chama cha wachimbaji kimetoa ombi hilo kwenye mkutano wa madini ya Tantalum-Niobium unaofanyika mjini Kigali.

    Mwenyekiti wa chama hicho Jean Malic Kalima, amesema ada ya juu ya ufuatiliaji inaathiri mchakato wa uchimbaji kwani wanatakiwa pia kulipa kwenye nchi za nje wanapouza madini.

    Kwa mwaka kampuni za madini hutumia hadi dola milioni 5 kama ada ya ufuatiliaji na kupata leseni husika.

    Mkurungezi wa madini, gesi na petrol wa Rwanda Francis Gatare, amesema ada ya juu ufuatiliaji inaathiri sekta hiyo na kusema kuwa inahitaji kupunguzwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako